Bunge la Ulaya laidhinisha makubaliano ya biashara huru na Japan
Wabunge wa bunge la Ulaya wameidhinisha makubaliano ya biashara yaliyofikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Japan leo, yakiondoa vizuwizi vya mwisho kwa makubaliano hayo kuanza kazi mapema mwaka ujao.
Makubaliano hayo, makubwa kuwahi kujadiliwa na Umoja wa Ulaya, yataunda soko la pamoja lenye watu wapatao milioni 600 mara litakapoanza Februari mosi , 2019.
Bunge la Japan tayari limeidhinisha makubaliano hayo ambayo yanaonekana kama karipio kwa sera za kulinda biashara za rais wa Marekani Donald Trump.
Chini ya makubaliano hayo, Japan itaondoa ushuru wa asilimia 94 kwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini humo kutoka Umoja wa Ulaya, wakati kundi hilo la mataifa litaondoa asilimia 99 ya ushuru wake kwa bidhaa zinazotoka Japan. Japan ina uchumi wa tatu mkubwa duniani, nyuma ya Marekani na China.
No comments