Breaking News

Waziri mkuu awashutumu wanaotaka kujitenga jimbo la Catalonia

Waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez leo amewashutumu wanaotaka kujitenga katika jimbo la Catalonia kwa kuelezea msingi wa hatua yao kwa uongo na kuwatumia watu, akiwafananisha na waungaji mkono wa Brexit nchini Uingereza. 

Akilihutubia bunge leo, amesema makundi yote ya harakati hizo yamejengeka katika malalamiko yakutungwa, na kukuzwa mno. 

Sanchez amesema wanaotaka kujitenga katika jimbo la Catalonia, wanasema uongo tu kutetea nafasi zao za kisiasa. 

Matamshi yake yanakuja wakati wabunge wa Uingereza wakianzisha kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Theresa May kuhusiana na mpango wa Brexit, na kuzusha mzozo mkubwa wa kisiasa dhidi yake tangu kuingia madarakani mwezi mmoja baada ya Waingereza kupiga kura Juni , 2016 kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.

No comments