Breaking News

Tetesi za Soka Barani Ulaya 13.02.2018. Pogba, Toure, Morata, Llorente, Bailly

Klabu ya Chelsea inapania kuiuzia Barcelona mshambuliaji wake Alvaro Morata, 26. (RAC1 - in Spanish)
Tottenham inajiandaa kuona endapo Real Madrid na Manchester United zitafufua nia yao ya kumchukua meneja wake Mauricio Pochettino mwisho wa msimu huu. (Guardian)
Juventus wana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kwa kima cha euro milioni 80 ifikapo mwezi Januari, ama watumie fedha hizo kufadhili uhamisho wa kiungo wa kati na mshambuliaji wa Real Madrid Isco, 26. (Tuttosport - in Italia)
Arsenal wana mpango wa kumsajijili beki wa kati mwezi Januari huku wakitafakari uwezekano wa kuwasajili kiungo wa Manchester United na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Eric Bailly, 24, nyota wa zamani wa kimataifa wa England Gary Cahill, 32, wa Chelsea na mlinzi wa Real Valladolid Fernando Calero, 23. (Mirror)
Mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, 33, amesema kuwa anajiandaa kurejea klabu yake ya zamani Athletic Bilbao baada ya kujikakamua kuacha alama yake Tottenham. (Evening Standard)
Mlinzi wa zamani wa Ivory Coast Yaya Toure, 35, anaamini kuwa bado anaweza kucheza katika ligi kuu ya England.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City aliondoka Olympiakos siku ya Jumatano na tayari amekataa ofa kutoka kwa Super League ya Uchina na vilabu vya vinavyoshiriki ligi ya MLS. (Sky Sports)
Mlinzi wa Barcelona Gerard Pique, 31, ameimarisha juhudi ya kununua klabu inayocheza ligi ya daraja la tano nchini Uhispania FC Andorra. (Diari d'Andorra - in Spanish)
Atlanta United inayoshiriki ligi ya MLS wamepinga tetesi kuwa wanamtafuta meneja wa Leeds United Marcelo Bielsa wanapojiandaa kumchagua kocha mpya. (Mail)
Kiungo wa kati wa Atlanta United kutoka Paraguay Miguel Almiron, 24, atawagharimu Arsenal au Newcastle zaidi ya euro milioni 30. (Mirror)
Real Madrid wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Argentina Exequiel Palacios, 20

No comments