Ligu ya Mabingwa Ulaya leo Napoli vs Barcelona, Chelsea vs Bayern
Ligi ya Mabingwa Ulaya leo inarejea tena ikiwa ni katika hatua ya mtoani (Knockout Stage). Leo Napoli watakuwa nyumbani wakiwakaribisha wafalme wa Hispani Barcelona, huku Chelsea pia wakiwa nyumbani kwao Stamford Bridge wakiwakaribisha Bayern Munich kutokea Ujerumani.
Napoli watashuka dimbani huku wakimkosa beki wao Kalidou Koulibaly ambaye ni majeruhi, na Barcelona pia bado wakimkosa mshambuaji wao Luis Suarez ambaye anatarajiwa kurejea dimbani mwishoni mwa msimu huu.
Huku Chelsea na Bayern Munich nao watashuka dimbani leo usiku, ifahamike kuwa mara ya mwisho wawili hao kukutana katika mashindano hayo ilikuwa ni mwaka 2012 kwenye fainali, na Chelsea akaimbuka mshindi kwa mikwaju ya penati 4-3.
Leo Frank Lampard kocha wa Chelsea, atahitaji ushindi ukiwa ni kitu kikubwa katika safari yake kama kocha lakini pia Bayern watahitaji ushindi wakikumbuka mara ya mwisho wawili hao walivyokutana na Bayern wakapoteza.
Nini maoni yako katika mechi za leo usiku, usisite kutoa comment, hapo chini
No comments