Breaking News

Champions League kupigwa Agosti, na kumalizikia Lisbon


Michuano ya msimu huu ya Ligi ya Klabu bingwa Ulaya, iliyosimamishwa tangu Machi kwa sababu ya janga la virusi vya corona, itakamilishwa mjini Lisbon, mweuzi Agosti.

Shirikisho la vyama vya kandanda barani Ulaya - UEFA limesema leo kuwa mashindano ya kile wanachokiita "Nane za mwisho" ambayo yatahusisha mechi za mkondo mmoja tu yataanza katika mji huo mkuu wa Ureno Agosti 12, na fainali kupigwa Agosti 23.

Aidha, michuano ya Europa League itamalizika katika muundo huo wa "Nane za Mwisho" ambapo itachezwa katika miji minne ya Ujerumani, Cologne, huku fainali ikipigwa Agosti 21. Hatua za mwisho za Champions League kwa wanawake itaendelea mjini Bilbao na San Sabastian mwishoni mwa mwezi huo.

No comments