Whatsapp kuja na hii 'Update' ambayo zaidi ya watu bilioni 2 duniani kote wanaisubiri
Najua utakubaliana na mimi kuwa Whatsapp ni moja ya mitandao maarufu sana duniani na ambayo inatumiwa na watu wengi sana. Karibia kila mtu mwenye smartphone, iwe Android au iPhone, lazima atakuwa na application hii kwani ni rahisi sana kutuma message na ina uaminifu wa hali ya juu.
Tangu mtandao huu ulivyoanzishwa, umekuwa ukikua siku hata siku na kuendelea kuimarika zaidi. Mpaka kufikia sasa, Whatsapp ndio mtandao wa mawasiliano mkubwa zaidi duniani kote. Maboresho ambayo mtandao huu umeweza kuyafanya mengine yanaweza yasionekane kama ni ya muhimu kama vile, kutunza (back up) message zako kwenye server zao ili zisipotee hata unapokuwa umenunua device mpya, kuweka muonekano wa giza (dark mode) ili kusaidia kuendelea kuwasiliana kwa urahisi wakati wa usiku. Lakini maboresho mengine yamekuwa makubwa zaidi, kama vile (end to end encryption) ambayo hii husaidia usiri wa mazungumzo ya watu, inamaana message za watu ambao wanachat, WhatsApp hawana uwezo wa kuziona hivyo kuendeleza usiri wa watumiaji. Lakini pia hivi karibuni wametangaza kuwa wanatarajia kuja na Whatsapp Pay ambayo hiyo itasaidia watu kutumiana pesa kupitia mtandao huo.
WhatsApp pia imeendelea kuaminiwa na wafanyabiashara wakubwa na hata baadhi ya taasisi za kiserikali pamoja na makampuni makubwa. Kupeana taarifa kwa njia ya WhatsApp kumeonekana kuwa rahisi na kuwafikia watu wengi kwa haraka ukilinganisha na mitandao mingine.
Bringing Payments to WhatsApp for People and Small Businesses in Brazilhttps://t.co/uvslFsImwc
— WABetaInfo (@WABetaInfo) June 15, 2020
Kama ambavyo siku zote huwa tunataarifiwa na Account ya "Whatsapp Beta Info" ambayo ndio account rasmi ya Whatsapp kwa ajili ya kutoa matangazo mbalimbali kuhusiana na mabadiliko na matengenezo ya mtandao huo, hivi karibuni account hiyo ilidokeza kuwa, WhatsApp iko mbioni kutengeneza feature mpya ambayo itahusisha kuunganisha (ku-link) mtandao katika device zote ambazo mtumiaji anazo kama vile simu, iPad, Desktop na Smartwatch. Lakini pia wataweza kuongeza idadi ya watu katika video calls, kwani hivi sasa unaweza kuongea na watu nane tu kwa wakati mmoja kwa kutumia video call, lakini hapo baadae idadi itaongezeka.
Linapokuja kwenye suala zima la message na usiri wake, WhatsApp ina faida kubwa na hupendelewa na watu wengi kama ambavyo nimeongelea muda si mrefu ukilinganisha na application kama Zoom na Google Meet na Teams. Whatsapp huendesha maisha yetu ya kila siku na hebu jaribu tu kufikiria kwamba endapo mtandao huu utaweza kutengeneza application ambayo itaweza kupakuliwa (download) kwenye computer na kuweza kulink na simu na kufanya mambo yote kama vile video call na mengine mengi, nadhani itakuwa na nafasi kubwa zaidi ya mitandao mingine.
No comments