China yapambana na mlipuko mpya wa corona jijini Beijing
Sehemu zote za ndani za michezo na burudani zimefungwa katika mji mkuu wa China wa Beijing hii leo, na baadhi ya mitaa wakazi wake wamelazimishwa kubakia majumbani mwao, huku serikali ikiwa inajaribu kudhibiti mripuko mpya wa virusi vya corona unaohusishwa na soko la chakula la Xinfadi.
Maelfu ya watu mjini Beijing pia wameanza kufanyiwa vipimo vya COVID-19, pamoja na kuwafuatilia wale wote waliokuwa karibu na soko hilo, huku idadi ya maambukizi mapya ikifika 79.
Kwa jumla watu 177 sasa wanaugua ugonjwa wa COVID-19 nchini China - wawili miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya. Idadi hiyo inatajwa kuwa ni ya juu zaidi tangu mapema mwezi Mei.
No comments