Breaking News

Mataifa ya Ulaya kulegeza udhibiti wa mipaka


Baadhi ya mataifa ya Ulaya yameanza kulegeza udhibiti wa mipaka yao hii leo, baada ya kufungwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona. Mipaka ilikuwa imefungwa kwa muda wa miezi mitatu katika eneo la Schengen la nchi 22 za Umoja wa Ulaya pamoja na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswisi, ambalo kawaida halizingatii udhibiti wa mipaka.

Kamishna wa Masuala ya Ndani ya Ulaya Ylva Johansson, alitoa wito kwa nchi wanachama wa Schengen wiki iliyopita, kuondoa udhibiti wa ndani wa mipaka ya Ulaya kuanzia leo Jumatatu, na kuruhusu tena mipaka kuwa wazi kwa nchi nyingine kuanzia mwezi Julai. Ingawa vikwazo vingi vya kusafiri katika kanda ya Schengen na eneo zima la Ulaya vitapunguzwa, usafiri hautakuwa wa kawaida kama ilivyokuwa zamani

No comments