OPEC yarefusha muda wa kupunguza uzalishaji mafuta
Kundi la mataifa yanayozalisha kwa wingi mafuta duniani OPEC limekubaliana kurefusha makubaliano ya kupunguza uzalishaji mafuta hadi mwezi Julai wakati bei ya nishati hiyo ikianza kuimarika na vizuizi dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 vikiendelea kupungua.
Kundi hilo la mataifa 13 pamoja na washirika wake ikiwemo Urusi limeridhia kurefusha kwa mwezi mmoja zaidi makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa mwezi April ya kupunguza kwa kiwango kikubwa uzalishaji mafuta ili kuvutia kuongezeka kwa bei.
Hata hivyo Mexico ambayo tayari ilitangaza kuwa haitofanya mabadiliko katika uzalishaji wake mafuta imesema haitatekeleza makubaliano yaliyofikiwa na OPEC. Chini ya makubaliano ya mwezi April mataifa ya OPEC na washirika wake waliahidi kupunguza uzalishaji mapipa milioni 9.7 kwa siku kwa mwezi Mei na Juni baada ya bei za nishati hiyo kuanguka kutokana na janga la virusi vya corona.
No comments