Breaking News

Kampuni ya Sony yatangaza ujio wa game mpya ya Black Ops 4

Kwa wale wapenzi wa gaming, Kampuni ya Sony imetangaza kuwa itakuwa inatoa game ya Black Ops3 kama zawadi kwa wale watu ambao watanunua game mpya ya Black Ops4 ambayo itatoka mwaka huu.

Kampuni hiyo imesema kuwa kutakuwa na ramani nne katika game hiyo mpya ambazo ni JUNGLE, SUMMIT, SLUMS na FIRING RANGE, lakini endapo utanunua game hiyo mpya itaweza kupewa zawadi ya Black Ops3 pamoja na ramani hizo mpya za kwenye Black Ops4 lakini utaweza kuzicheza kwenye Black Ops3. 

Game hiyo inatarajiwa kuwa ya kusisimua sana kutokana na graphics zake, lakini pia itakuwa na majina halisi ya ramani na sehemu ambazo game hiyo itakuwa inachezwa na inatarajiwa kutoka October 12. 

No comments