Breaking News

Belgium wawakatia tiketi Tunisia, South Korea chali kwa Mexico

Katika mchezo uliopigwa jana katika dimba la Otkrytika Arena kati ya Belgium na Tunisia, Belgium waliweza kuwakatia tiketi Tunisia baada ya kuwafunga mabao 5-2. Mabao hayo yaligungwa na Eden Hazard(2), Romelu Lukaku(2) na Mitchy Batshuayi(1) huku magoli ya Tunisia yakiwa yamefungwa na Dylan Bronn na Wahbi Khazri(1). Belgium sasa watakuwa ndio viongozi wa kundi G wakiwa na point 6 na magoli 8.
Mchezo mwingine ulikuwa kati ya South Korea dhidi ya Mexico, mchezo ambao ulimalizika kwa timu ya taifa ya Mexico kushinda mabao 2-1. Mabao ya Mexico yalifungwa na Carlos Vela na Javier Hernandez maarufu kama Chicharito, huku bao pekee la South Korea likifungwa na Heung Min Son. Mexico wanakuwa ndio viongozi wa kundi F wakiwa na Point 6 na mabao 3.

No comments