Breaking News

England waicharaza Panama mabao 6-1, Harry Kane aongoza kwa magoli

Baada ya kuanza vyema kwenye mechi yao ya ufunguzi kwa kuwachapa Tunisia mabao 2-1, Timu ya taifa ya England imeendeleza ubabe wake mbele ya Panama baada ya kuwachapa mabao 6-1. Mabao ya England yamefungwa na John Stones dk 8', Harry Kane dk 22', Jesse Lingard dk 36', John Stones dk 40', Harry Kane dk 45+1', na Harry Kane akimalizia tena dk 62'. Bao pekee la Panama limefungwa na Felipe Baloy dk 78'. 
Harry Kane sasa anakuwa mchezaji wa pili kushinda Hat trick kwenye mechi ya Kombe la Dunia baada ya Cristiano Ronaldo kufanya hivyo dhidi ya Spain, huku tayari akiwa ndiye mfungaji bora mpaka sasa akiwa na mabao 5 akifuatiwa na Romelu Lukaku na Diego Costa. England sasa wamejihakikishia kwenda hatua ya 16 bora wakiwa na point 6 na magoli 8 sawa na Belgium. 

No comments