Beyonce na Jay Z watoa album mpya "Everything Is Love"
Staa wa muziki nchini Marekani Beyonce ameweza kuwashangaza mashabiki zake tena baada ya kutoa album pasipo wao kutegemea lakini mara hii aliweza kupata usaidizi kutoka kwa mume wake Jay Z.
Wawili hao waliweza kutoa album hiyo inayojulikana kama "Everything Is Love" iliyotoka siku ya Jumamosi katika mtandao wao wa Tidal. Project hiyo imeweza kuchukua muda mrefu kidogo na imekuja kipindi ambacho wawili hao wakiendelea na ziara (On The Run II) yao barani Ulaya ambayo itaendelea marekani mwezi Julai.
Mwimbaji huyo aliweza kutoa kionjo cha album hiyo kwa kupitia nyimbo inayojulikana kama "Ape S**t" ambayo iliweza kutengenezwa mwezi Mei wakiwa jijini Paris nchini Ufaransa.
Beyonce pia aliweza kuweka wazi vitu vingine kuhusiana na album hiyo ikiwemo cover art ya album hiyo katika ukurasa wake wa Instagram.
Wawili hao wamekuwa wakitoa album mara nyingi kuhusiana na mahusiano yao na maisha yao ya ndoa na changamoto wanazopitia na kuhusiana na wanavyozikabili ili kuweza kudumisha mahusiano yao.
No comments