Breaking News

Kifaa maalumu chatabiri nani atashinda kombe la Dunia


Kombe la Dunia linatarajia kuanza hapo kesho nchini Russia huku timu mbalimbali zikiwa zimeshawasili kama vile Brazil, Egypt, Iran, Ufaransa na nyingine nyingi. Yanatazamiwa kuwa mashindano makubwa sana hata kupita mashindano ya Olimpic kwa hiyo kila timu itafanya kila liwezekanalo kunyakua kombe hilo.

Lakini huku tukiwa tunasubiri kwa hamu kuanza kwa mashidano hayo kuna makampuni baadhi ambayo hayo hutumia watu waliobobea kwenye masuala ya takwimu ili kutambua ama kubashiri ushindi kati ya timu zinazocheza hata kabla ya mechi husiku kuanza. Kwa kutambua hilo, ndipo wanapoweza kuweka ubashiri wao na kuweka "odds" ili watu wengine waweze kubashiri pia.

Kwa kupitia njia hiyo na mfumo huo wa kubashiri, vifaa hivyo vimeweza kubashiri kuwa timu ya taifa ya Brazil ina nafasi kubwa ya kushinda kombe hilo kwa wastani wa 16%, ikifuatiwa na Ujerumani 12.8% na Uhispania 12.5%. 

Mashindano hayo yanatarajia kuanza Juni 14, 2018 huku wenyeji, Russia wakiwa ndio wafunguzi dhidi ya Saudi Arabia. Jambo ambalo ni la kusikitisha na kushangaza sana ni kwamba wawili hawa wote hakuna anayeonekana kama ataweza kufikia mbali.

No comments