Mamia wajitokeza mitaa ya London kupinga Brexit
Maelfu ya watu wamemiminika katika mitaa ya London leo Jumamosi, kupinga hatua ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya, ikiwa imetimia miaka miwili baada ya nchi hiyo kuushangaza ulimwengu katika matokeo ya kura ya maoni ya Brexit.
Maandamano hayo yaliandaliwa na kundi la wanaopinga Brexit na likijaribu kushinikiza kufanyika kwa kura ya umma juu ya mkataba wa mwisho wa kujiondoa umoja huo utakaokubaliwa na muungano wa Ulaya.
Tukio la Jumamosi lilihudhuriwa na wanasiasa wanaounga mkono Umoja wa Ulaya kutoka pande tofauti za kisiasa nchini Uingereza ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha Labour, Liberal Democrats na baadhi ya wanachama kutoka chama cha kihafidhina cha Waziri Mkuu Theresa May wanaopinga Brexit.
No comments