Mke wa Benjamin Netanyahu ashtakiwa kwa ulaghai
Mke wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, bi Sara ameshtakiwa kwa ulaghai na kuvunja uaminifu, kufuatia uchunguzi wa muda mrefu wa maafisa wa polisi dhidi ya madai ya udanganyifu kuhusu gharama ya matumizi ya nyumbani.
Hayo yamesemwa na wizara ya sheria ambayo imeongeza kuwa tayari mkuu wa mashtaka wa wilaya ya Jerusalem, amefungua mashtaka dhidi ya bi Sara. Madai hayo yaliyotolewa mwaka jana, yanasema bibi Sara na msaidizi wake walitoa maelezo ya kupotosha kuwa hakukuwa na wapishi katika makaazi rasmi ya waziri mkuu, hivyo waliamuru wapishi kutoka nje waliogharamiwa kwa fedha za umma.
Wizara ya haki imesema gharama hizo zilifikia dola 97,000. Sara ameyakana madai hayo. Mume wake pia anachunguzwa kwa makosa ya rushwa.
No comments