Breaking News

Mtandao wa "WhatsaApp" utaacha kutumika katika simu zifuatazo


Mtandao wa Whatsapp umetangaza rasmi kuwa utaacha kutumika kwa baadhi ya simu baada ya miaka miwili ijayo yaani 2020. Mtandao huo unaomilikiwa na Facebook mpaka sasa una zaidi ya watumiaji bilioni 1.5 dunia nzima. 

Katika kulielezea jambo hilo mtandao huo umesema kwamba utasitisha matumizi yake katika system zifuatazo. 
  • Wale wenye simu za iPhone (zenye iOS 7 kushuka na kushuka chini)
  • Wale wenye simu za Android (zenye android version ya 2.3.7 maarufu kama Gingerbread na kushuka chini)
Watumiaji wa system hizo mbili hawataweza kutengeneza tena account mpya za Whatsapp, bali wataweza kutumia hizo walizokuwa nazo sasa mpaka kipindi hiko cha miaka miwili kitakapoisha kisha watashindwa kutumia mtandao huo tena, isipokuwa watanunua simu mpya zenye operating system ambazo zinauwezo wa juu kuliko zilizoelezwa hapo awali. 

Android Gingerbread ilitengenezwa mwaka 2010 na bado ina watumiaji 0.3 katika soko la simu za Android ambapo ukifanya hesabu za harakaharaka utagundua kuwa bado kuna watumiaji karibia milioni 6 ambao bado wanatumia system hizo. 

Kama bado unatumia operating system hizo mtandao huo unakusihi ubadilishe na kuanza kutumia system zifuatazo.
• Android version kuanzia 4.0 na kuendelea
• iPhone (iOS 8 na kuendelea)
• Window version kuanzia 8 na kuendelea

No comments