Wakati wakiivaa Croatia hii leo, Mama Messi aeleza masikitiko yake
Kati ya habari kubwa tangu michuano ya kombe la dunia ianze ni tukio la nyota wa Argentina Lionel Messi kukosa tuta katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Argentina.
Tangu Messi akose penati kumekuwa na maneno mengi mabaya juu yake na mashabiki wa timu ya taifa ya Argentina pia wamekuwa wakimshambulia sana kwa maneno mchezaji huyo wa Barcelona.
Celia Cucittini ni mama mzazi wa Lionel Messi na anaona kinachoendelea kwa sasa kuhusu mwane na kueleza kusikitishwa na hali hiyo huku akisema Messi anaumia sana kwa hali hii ya sasa.
Ameeleza kwamba maneno ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa mwanaye yamekuwa yakiathiri kiwango chake moja kwa moja na kuwataka watu watambue kwamba Messi analipambania taifa.
“Kama kuna mtu anataka kurudi na kombe nyumbani baasi namba moja ni Leo, kombe la dunia limekuwa ndoto yake kubwa na anatoa kila alichonacho kupata kombe hilo” alisema Celia.
Kumekuwa na hali ya kutokuelewana kwa muda sasa kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina na vyombo vya habari nchini kwao hali inayopelekea mara nyingi kwa vyombo hivyo kuishambulia timu yao ya taifa pindi ikiboronga.
Hadi sasa Argentina wana alama moja tu katika kundi lao D na hii leo watakipiga dhidi ya Crotia huku Gabriel Mercado akionya kwamba Messi ana njaa kali ya kumwadhibu yeyote atakayesogea mbele ya Argentina kwa sasa.
Wakati mwaka 1998 ikiwa mara ya mwisho kwa Croatia kushinda mechi mbili mfululizo kombe la dunia, Argentina wenyewe hawajawahi kupoteza mechi mbili mfululizo za mwanzo tangu mwaka 1974.
Timu hizi mbili zimeshawahi kukutana mara nne huku Argentina wakiipiga Croatia mara mbili, Croatia wakipata ushindi mara moja na mara moja iliyobaki wakipata suluhu.
No comments