Real Madrid wamemtangaza Julen Lupetegui kama kocha wao mpya baada ya Zidane kuondoka
Klabu ya Real Madrid ya Hispania imemtangaza Julen Lupetegui kama kocha mpya wa klabu hiyo baada ya aliyekuwa kocha wao Zinedine Zidane kuondoka klabuni hapo.
Ikumbukwe kuwa Zinedine Zidane aliondoka klabuni hapo baada ya kuifundisha timu hiyo kwa muda wa miaka miwili na nusu alishinda mataji mengi yakiwemo ya UEFA Champions League kwa misimu mitatu mfululizo akiweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya mpira wa miguu na kuweka rekodi nyingine kuwa kocha aliyewahi kuchukua kombe hilo akiwa kama kocha na akiwa kama mchezaji.
No comments