Sterling: Mtoto wangu wa kike sio shabiki wa Manchester City
Mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling amesema kwamba licha ya kuwa na mafanikio mazuri na ushindi mnono wa ligi kuu ya Uingereza akiwa na Manchester City, mtoto wake wa kike ni mshabiki wa Liverpool damudamu, timu ambayo alikuwa akiichezea mshambuliaji huyo hapo awali.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza aliweza kutengeneza historia katika msimu uliopita na kuwafurahisha watu wengi wakiwemo mashabiki zake lakini mtoto wake wa kike hakuwa mmoja wao.
Washindi hao wa ligi kuu ya nchini Uingereza, walikuwa timu pekee ya kwanza kufikia idadi ya point 100 katika msimu baada ya kuongoza ligi hiyo na kutwaa taji katika mwezi April 2018.
Licha ya kuwa msaada mkubwa sana wa timu yake ya klabu, akiwa amefunga mara 18, wakiwa wameshinda taji la ligi kuu na kombe la EFL, bado mchezaji huyo hakuweza kumshawishi mwanae kubadilisha timu yake(Liverpool) ili kuishabikia Manchester City.
No comments