Breaking News

Umoja wa Ulaya waanza kutekeleza kodi kwa bidhaa za Marekani

Umoja wa Ulaya umeanza kutekeleza kodi kwa bidhaa muhimu zinazotoka Marekani zikiwemo pikipiki, suaruali za jeans na mvinyo, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi ambayo inaanzisha vita vya kibiashara na Rais Donald Trump wa Marekani. 

Kodi hizo, ambazo zilianza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, itazusha wasiwasi katika masoko ya hisa kote duniani ambayo tayari yanafuatilia kwa karibu mvutano huo wa kibiashara kati ya Marekani na China. 

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema hatua hizo za Ulaya zinaonyesha kuwa Umoja wa Ulaya uko imara na unafuata misingi yake. Trump alitangaza kodi kubwa kwa idhaa za chuma cha pua na bati zinazoingizwa Marekani kutoka Ulaya.

No comments