Rais wa China aanza ziara yake ya wiki nzima Mashariki ya Kati na Afrika
Rais wa China Xi Jinping ameondoka leo kuanza ziara ya wiki nzima ya Mashariki ya Kati na Afrika kabla ya mkutano wa kilele wa10 wa kundi la nchi zinazoinukia kiviwanda duniani - BRICS nchini Afrika Kusini wiki ijayo. Xi kwanza ameelekea katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara fupi ya kiserikali kabla ya kuelekea Senegal, Rwanda na kisha Afrika Kusini ambako atahudhuria mkutano wa BRICS mjini Johannesburg na viongozi wa Brazil, Urusi, India na Afrika Kusini.
China ni mshirika mkubwa kabisa wa kiuchumi barani Afrika, ambapo kuna zaidi ya makampuni 10,000 ya kichina yaliyosambaa kote barani humo. Kuongezeka kwa ushawishi wa China barani Afrika umeibua maswali, hasa nchini Marekani, ya kama bara hilo limeanza kuona aina mpya ya ukoloni wa kiuchumi.
Post Comment
No comments